SHINIKIZO ZA KUONGEZA MUDA WA USAJILI WA WAPIGA KURA ZAENDELEA KUTOLEWA.

Na Benson Aswani

Shughuli ya kuwasajili wapiga kura wapya ikitarajiwa kukamilika rasmi hii leo kundi moja la vijana katika kaunti ya baringo sasa wanairai tume ya uchaguzi nchini iebc kuongeza muda wa usajili.
Wakiongea kwenye eneo la Kaploten vijana hao wakiongozwa na Enock Barnoo na titus ng’etich wamesema kuwa kuongezwa kwa mda huo kutatoa nafasi kwa vijana kote nchini kujisajili kama wapiga kura.
Barnoo amesema kuwa vijana watakuwa na usemi mkubwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao hivyo pana haja ya kupewa muda wa kushiriki kwenye shughuli ya usajili.
Hata hivyo vijana hao wameelezea kusikitishwa na idadi ndogo ya vijana ambao imejitokeza ili kushiriki kwenye zoezi hilo wakisema kwamba ndio watakaoendelea kuumia iwapo hawatajisajili kuwa wapiga kura.