SHILINGI MIA SITA YASABABISHA MUME KUMUA MKEWE

KAKAMEGA


Mwanamme mwenye umri wa miaka 60 anazuiliwa na maafisa wa polisi katika eneo bunge la Shinyalu kwenye kaunti ya Kakamega kwa tuhuma za kumuua mkewe mwenye umri wa miaka 57 kufuatia mzozo wa shilingi mia sita.
Kulingana na wakazi,mshukiwa Joseph Omulabu alimpiga mkewe kwa silaha butu.
Familia ya marehemi inasema kwamba mshukiwa amekuwa na tabia ya kumpiga mkewe mara kwa mara.
Kufutia kisa hicho familia ya mshukiwa inasema kwamba kulingana na mila na tamaduni ya jamii hiyo haitamruhusu kurudi kutangamana na familia yake tena.