SHILINGI HAMSINI YASABABISHA MAUTI

POKOT MAGHARIBI


Vijana wawili mjini Makutano kwenye Kaunti ya Pokot Magharibi ambao wamekuwa wakifanya kazi ya kubeba mizigo wamefariki papo hapo baada ya kugombania shilingi hamsini.
kulingana na walioshuhudia kisa hicho, Vijana hao walipigania pesa hizo kabla ya mmoja wao kuchomoa kisu na kumdunga mwenzake kifuani na kumwacha akiwa amekata roho kabla yeye kuvamiwa na Raia Waliojawa na ghadhabu.
Maafisa wa polisi wa kituo cha Kapenguria waliubeba Miili hiyo huku wakifanikiwa kukiokota kisu kilichotumika kwa mauaji hayo na kupisha uchunguzi zaidi wa kisa hicho.