SHARTI LA KUTOKUWA NJE LAOMBWA KUONDOLEWA NA VIONGOZI WA KIDINI


Viongozi wa kidini kwenye kaunti ya Uasin Gishu wameiomba serikali kuondoa sharti la kutokuwa nje kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri wakati wa sherehe za mwaka mpya
Wakiongozwa na mwenyekiti wao askofu Wilson kurui wa kanisa la Jesus Love Ministries na Bonface Simani wamesema waumini wa dini mbalimbali wanapaswa kutumia mkesho wa mwaka mpya kuliombea taifa wa mwaka wa alfu mbili ishirini na moja unapoanza.
Wamemwomba rais uhuru kenyata na naibu wake wiliam ruto kuitafakari ombi lao kwa kuwa wakenya wanastahili kujumuika na kufanya maombi
Wakati huo dhidi ya janga la corona vilevile changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikilikumba taifa hili aidha wametaka masharti mengine yaendelee kutekelezwa.