SERKALI YA GAVANA LONYANGAPUO YASUTWA NA SENETA POGHISIO
Seneta wa kaunti hii ya Pokot Magharibi Samwel Poghisio ameendelea kuisuta serikali ya gavana John Lonyangapuo kuhusu jinsi ambavyo inashughulikia maswala mbali mbali yanayowakumba wakazi wa kaunti hii.
Akirejelea visa vya kuteketea bweni la shule ya msingi ya Tartar na sehemu ya soko la makutano, Poghisio amesema kuwa hamna hatua zozote ambazo zimechukuliwa na serikali ya gavana Lonyangapuo licha madhara ambayo yalisababishwa na mikasa hiyo ya moto.
Poghisio amesema serikali ya kaunti hii haina mikakati yoyote ambayo imeweka kukabili majanga yanapotokea.
Wakati uo huo Poghisio amemsuta gavana Lonyangapuo kufuatia madai ya kuendelea kuwalipa mshahara maafisa waliokuwa wakihudumu katika serikali ya kaunti licha yao kujiuzulu akisema swala hilo linachunguzwa na idara husika.