SERKALI KUU YATARAJIWA KUKAMILISHA MIRADI ILIYOANZISHA

POKOT MAGHARIBI


Seneta wa kaunti hii ya Pokot magharibi samwel poghisio ameipongeza serikali kuu kwa miradi ambayo ilianzisha kaunti hii ili kuwanufaisha wakazi.
Akizungumza baada ya kukagua miradi mbali mbali, poghisio ambaye alikuwa ameandamana na maafisa wengine serikalini akiwemo katibu wa wizara ya ugatuzi Mika powon, amesema miradi hasa ule wa maji wa siyoi muruny utasuluhisha tatizo la maji ambalo limekumba mji wa makutano na viunga vyake kwa muda sasa.
Aidha poghisio amesema kutekelezwa miradi hii katika kaunti hii na maeneo mengine ya nchi itafanya rahisi kuuza sera za mpango wa upatanishi BBI ambao kufikia sasa idadi hitajika ya mabunge ya kaunti kuidhinisha mswada wa marekebisho ya katiba imeafikiwa.
Kwa upande wake katibu katika wizara ya ugatuzi Mika powon amesema miradi hiyo ikiwemo ujenzi wa barabara mbalimbali imeendelea vyema licha ya changamoto zinazoshuhudiwa akiwaahidi wakazi wa kaunti hii kuwa serikali itahakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati unaofaa.
Maafisa wengine walio hudhuria hafla hiyo ni pamoja na kamishna wa kaunti hii Apollo okelo katibu belio kipsang anayehudumu katika idara ya maeneo kame,katibu Andrew kamau wa madini na petroli miongoni mwa maafisa wengine wa serikali.