SERKALI KUU YAANZISHA MPANGO WA UJENZI WA CHUO CHA UTABIBU TRANSNZOIA ENEO LA CHERANGANYI


Serikali imeanzisha mpango wa ujenzi wa chuo cha mafunzo ya utabibu katika eneo la cherang’ani kaunti ya Trans nzoia ikiwa njia moja ya kuhakikisha kwamba huduma bora za afya zinafika eneo hilo.
Kamati ya afya katika bunge la kitaifa imezuru maeneo hayo kutafuta maoni ya wakazi kuhusu idadi ya wanafunzi wanaotafuta elimu ya utabibu katika meneo mengine nchini.
Kamati hiyo imebaini kwamba jumla ya wanafunzi alfu 30 waliokamilisha masomo ya shule za upili hutuma maombi ya kutafuta nafasi katika vyuo vya utabibu hali inayofanya kuwa vigumu hasa ikizingatiwa idadi ya wanafunzi kote nchini.
Kulingana na kamati hiyo ni asilimia 50 pekee ambayo hupata nafasi hizo hali ambayo imelazimu serikali kuanzisha ujenzi wa chuo hicho katika eneo la kachibora cherang’ani.
Naibu mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni mbunge wa Cherang’ani Joshua Kutuny amesema kuwa zaidi ya shilingi milioni 7 zimetengwa ili kufanikisha mradi huo.