SERIKALI YATANGAZA OPARESHENI YA KUTWAA SILAHA HARAMU KERIO VALLEY.


Serikali imetangaza kuanza oparesheni ya kutwaa silaha ambazo zinamilikiwa kinyume cha sheria katika kaunti za Elgeyo marakwet na Baringo kufuatia utovu wa usalama unaoshuhudiwa katika kaunti hizo.
Oparesheni hii inafuiatia mauaji ya watu wanne kwenye mpaka wa kaunti hii ya Pokot magharibi na Elgeyo marakwet tarehe moja mwezi huu.
Waziri wa maswala ya ndani ya nchi Dkt Fred Matiangi amesema kuwa oparesheni hiyo inalenga kuhakikisha usalama unarejelewa na kuwaruhusu wanafunzi kurudi shuleni kwani baadhi ya shule zimesalia kufungwa licha ya masono kurejelewa kote nchini kuanzia januari tarehe nne.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na mshirikishi wa utawala katika eneo la bonde la ufa George Natembeya.
Natembeya amesema kuwa serikali haitawasaza wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kwani ni tishio kwa usalama wa wananchi.