SERIKALI YATAKIWA KUZIDISHA OPARESHENI YA KIUSALAMA MUKUTANI, BARINGO


Wakazi wa eneo la Mukutani, eneo bunge la baringo kusini kaunti ya baringo wanaitaka serikali kuharakisha oparesheni ya kutwaa silaha haramu na kuwakabili wezi wa mifugo.
Mmoja wa wakazi eneo hilo Harrison ole Meiguran anasema kuwa oparesheni hiyo inastahili kulenga baadhi ya maeneo ya eneo bunge hilo na eneo bunge la Tiaty ambako wavamizi wanaamikina kujificha.
Ole meiguran ameongeza kuwa wenyeji eneo hilo wanaendelea kuishi kwa wasi wasi ya kushambuliwa na wavamizi hao ambao wamekuwa wakiiba mifugo na kutekeleza mauaji kwa miaka mingi sasa.
Aidha meiguran amekosoa oparesheni za awali akisema kwamba maafisa wa usalama hawakufika hadi kwenye maeneo kunakoaminika kuwa maficho ya wezi wa mifugo.