SERIKALI YATAKIWA KUWEKA MIKAKATI YA KUKABILI UTOVU WA USALAMA BARINGO.


Serikali kuu kwa ushirikiano na ile ya kaunti ya Baringo imetakiwa kubuni mikakati itakayowezesha utekelezaji wa miradi tofauti ya maendeleo katika eneo bunge la Tiaty ambalo kwa muda limekumbwa na tatizo la wizi wa mifugo na utovu wa usalama.
Wakizungumza wakati wa mkutano wa kujadili maendeleo ya jamii ya eneo hilo, Nachale Kipchumba mkazi wa Tanglubei amesema kuwa hali ya usalma itarejea kwenye eneo bunge hilo iwapo tofauti itatekelezwa.
Kipchumba amesema kuwa kwa sasa watu wengi wametoroka makwao huku nao wafanya biashara wanalazimika kufunga shughuli zao mapema kwa hofu ya kuvamiwa.
Aidha Kipchumba ameomba serikali kuu kuimarisha juhudi zake za kurejesha amani katika eneo hilo hali anayosema itawavutia wawekezaji wengi hivyo kuimarisha uchumi wa eneo hilo.