SERIKALI YATAKIWA KUWEKA MIKAKATI KUKABILI BAA LA NJAA POKOT MAGHARIBI


Miito imeendelea kutolewa kwa serikali kuweka mikakati ya kuwasaidia wakazi wa maeneo mbali mbali ya kaunti hii ya Pokot magharibi kutokana na makali ya baa la njaa ambalo linawakodolea macho.
Wakiongozwa na Mark Bilil, wakazi wa kaunti hii wamesema kuwa uchache wa mvua ambayo imeshuhudiwa mwaka huu umepelekea kuathirika mimea ya wakulima wengi na sasa hawatarajii mavuno ya kutosha kama miaka ya awali.
Aidha wameelezea wasiwasi hasa wakati huu ambapo wanafunzi wanatarajiwa kufunga shule.
Wakati uo huo wakazi hao wamewashutumu viongozi wa kisiasa katika kaunti hii ya Pokot magharibi kwa kutoa kipau mbele kwa maswala ya kisiasa hali wapo wenyeji wengi ambao wanahangaika kwa kukosa chakula.