SERIKALI YATAKIWA KUWALINDA WAKAZI DHIDI YA ATHARI ZA MAFURIKO ILNG’ARUA BARINGO.


Wakazi wa eneo la ilng’arua katika kaunti ya baringo sasa wanaiomba serikali kuchukua hatua za mapema ili kuhakikisha hakuna maisha yanayopotea msimu huu wa mvua.
Kauli yao inajiri baada ya watoto wanne kunusurika kifo huku zaidi ya watu 1000 kutoka eneo hilo wakipitia changamoto za usafiri kufuatia mto perkera kuvunja kingo zake na kusomba daraja linalounganisha longewan na ilng’arua.
Kulingana na wakazi hao mvua kubwa iliyonyesha kwa muda wa saa 8 katika nyanda za juu za baringo pia imesababisha kusombwa kwa zaidi ya ng’ombe 80 kutokana na mafuriko.
Mafuriko hayo pia yamesababisha mazao yaliyozalishwa kutofika sokoni kwa wakati kwani wakazi wanategemea daraja hilo.
Eneo bunge la baringo kusini ndilo hukumbwa pakubwa na mafuriko haswa ngambo, salabani, longewan miongoni mwa maeneo mengine wakati wa mvua.