SERIKALI YATAKIWA KUWAHAKIKISHIA WAKAZI WA BARINGO USALAMA.


Mwakilishi wa wadi ya Bartabwa katika eneo bunge la Baringo kaskazini kaunti ya Baringo Reuben Chepsongol ametoa wito kwa serikali kuwahakikishia usalama wao wakazi wa kaunti hiyo kutokana na uvamizi wa mara kwa mara unaotekelezwa na wezi wa mifugo kila kukicha.
Akiongea na wanahabari mjini Kabarnet, Chepsongol amelaani kisa cha hapo jana ambapo mwanamke mmoja alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na wezi wa mifugo katika eneo la Ng’aratuko, miezi michache baada ya afisa wa serikali na wanafunzi kuuwawa katika eneo la kapturo.
Kulingana na Chepsongol serikali imezembea katika majukumu yake ya kuhakikisha wakazi wanapata ulinzi kwa mjibu wa katiba huku akiwalaumu viongozi kwa kusalia kimya wakati ambapo wananchi wanaendelea kupitia masaibu mengi
Wakati uo huo ameitaka serikali kuanzisha oparesheni ya kutwaa silaha haramu mikononi mwa wakazi kama ilivyofanyika katika kaunti ya samburu.