SERIKALI YATAKIWA KUTUMA FEDHA ZA CDF BAJETI IKISOMWA LEO.


Waziri wa fedha Ukur Yattani akitarajiwa leo kusoma bajeti ya kipindi cha mwaka 2021/2022, wito umetolewa kwa serikali imetakiwa kutuma fedha za maendeleo ya maeneo bunge ya kipindi cha fedha cha mwaka 2020/2021.
Mbunge wa kapenguria kaunti hii ya pokot magharibi samwel Moroto amesema kuwa ipo miradi mingi ambayo imekwama kutokana na ukosefu wa fedha kufuatia hatua ya serikali kuchelewa kutuma fedha hizo.
Moroto amesema kuwa serikali ilipasa kuhakikisha kuwa inatoa fedha hizo kwa maeneo bunge kabla ya kusomwa bajeti nyingine, huku akiibua maswali kuhusu inakokoenda mikopo ambayo serikali inachukua kutoka mashirika ya kutoa mikopo hiyo.