SERIKALI YATAKIWA KUKOMESHA UVAMIZI WA MARA KWA MARA BARINGO KASKAZINI NA KUSINI.


Serikali kuu kupitia asasi zake mbali mbali imetakiwa kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini kiini cha mashambulizi ya mara kwa mara kwenye eneo bunge la Baringo kaskazini na kusini katika kaunti ya Baringo.
Kulingana na mwaniaji wa wadhifa wa ubunge eneo bunge la Baringo ya kati Dr. Emily Kiptui huenda uvamizi wa sasa hauambatani na wizi wa mifugo kama miaka ya hapo nyuma.
Akizungumza na wanahabari Dr. Kiptui amedai kwamba kuna uwezekano mashambulizi hayo ambayo yamepelekea mamia ya watu kutoroka makwao yamechangiwa na mzozo wa mipaka na pia raslimali.
Hata hivyo kiptui amesema serikali inafaa kutumia mbinu zote kuwatia mbaroni wanaohusika na uvamizi hao na kuhakikisha kwamba amani na utulivu inarejea kwenye maeneo hayo.