SERIKALI YATAKIWA KUJENGA DARAJA KWENYE MTO SHALPO.


Wakazi wa eneo la shalpo katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametoa wito kwa serikali ya kaunti hii kujenga daraja kwenye mto wa eneo hilo litakalowawezesha kuvuka bila wasiwasi hasa wakati huu ambapo kumeendelea kushuhudiwa mvua kubwa.
Wakazi wa eneo hilo wakiongozwa na Francis Lomuria wamesema kuwa gavana Lonyangapuo aliahidi kujenga daraja hilo ila hadi kufikia sasa hilo halijatekelezwa, na sasa mto huo umeanza kuleta madhara hasa baada ya mama mmoja kusombwa na maji usiku.
Lomuria amesema kuwa kufurika mto huo kumetatiza huduma nyingi muhimu ikiwemo usafiri na hata kutoa wakati mgumu kwa wagonjwa kufikia huduma za matibabu, waathiriwa wakuu wakiwa kina mama na watoto.