SERIKALI YATAKIWA KUIWEZESHA KIFEDHA TUME YA TSC.


Serikali imetakiwa kuiwezesha kifedha tume ya huduma za walimu TSC ili kuwaajiri walimu zaidi kuendena na mpango wa kufanikisha wanafunzi wote ambao wanafanya mtihani wa KCPE kujiunga na shule za upili.
Katibu wa chama cha walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri kuppet tawi la Trans nzoia Furaha Lusweti aidha ameitaka serikali kuimarisha miundo msingi katika taasisi zote za elimu ili kuafikia sharti la umbali wa mita moja unusu ili kudhibiti msambao wa virusi vya corona miongoni mwa wanafunzi, walimu na hata wafanyikazi.
Wakati uo huo Lusweti amemwomba waziri wa elimu prof. George magoha kuongeza mgao unaotumwa kwa shule kutoka shilingi alfu 22 hadi alfu 30 ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi ambo wanatoka katika familia zisizojiweza.