SERIKALI YATAKIWA KUIMARISHA USALAMA POKOT NA MARAKWET
Viongozi kaunti ya Pokot Magharibi wameendelea kuishinikiza serikali kuimarisha usalama maeneo ya Kamologon kwa kuhakikisha kwamba maafisa zaidi wa usalama wanatumwa eneo hilo ambako watu wawili wameuliwa hivi majuzi na wezi wa mifugo.
Wa hivi punde kutoa wito huo ni mwakilishi wadi ya Lelan James Kapelo ambaye amesema kwa sasa shughuli muhimu zimesitishwa eneo hilo kufuatia utovu wa usalama ambapo pia limesalia pakubwa nyuma kimaendeleo.
Aidha Kapelo amehimiza ushirikiano baina ya idara za usalama katika pande zote mbili za kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jirani ya Elgeyo marakwet ili kuzidisha juhudi za kuimarisha usalama maeneo ya mipakani.