SERIKALI YATAKIWA KUIMARISHA USALAMA MIPAKANI PA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI NA ELGEYO MARAKWET.


Serikali imetakiwa kuweka mikakati ya kuhakikisha usalama unaafikiwa maeneo ya mpakani pa kaunti hii ya pokot magharibi na kauntijirani ya Elgeyo marakwet ili kuruhusu kurejelewa shughuli za masomo maeneo hayo.
Seneta wa kaunti hii ya pokot magharibi Samwel poghisio amesema kuwa hali ilivyo sasa si salama kwa wananfunzi na walimu kurejelea masomo licha ya serikali kuahidi kuimarisha usalama kwa kuwaleta maafisa zaidi wa usalama maeneo hayo.
Poghisio amesema kuwa kufikia sasa shule nyingi maeneo hayo hazijafunguliwa huku akipendekeza kuwekwa maafisa wa usalama katika shule zote eneo hilo ili kuwaondolea hofu ya kushambuliwa wanafunzi na walimu wanapoelekea shuleni.