SERIKALI YATAKIWA KUIMARISHA USALAMA KATIKA BONDE LA KERIO.

NA BENSON ASWANI
Viongozi kutoka eneo bunge la Marakwet magharibi kaunti ya Elgeyo marakwet wameendelea kashifu uvamizi uliotekelezwa na wahalifu katika eneo la chepkum katika wadi ya arror ambapo watu watatu walijeruhiwa wakiwemo wanafunzi wawili.
Wakiongozwa na mbunge wa eneo hilo William Kisang, viongozi hao wamesema serikali inapaswa kuhakikisha amani inadumu katika bonde la kerio huku wakihimiza haja ya viongozi kukutana na kutafuta suluhu ya kudumu kwa tatizo hilo.
Aidha viongozi hao wameelezea kuunga mkono pendekezo la kufanyika oparesheni ya kutwaa silaha haramu zinazomilikiwa na wakazi katika eneo la bonde la kerio.