SERIKALI YATAKIWA KUIMARISHA USALAMA KATIKA BONDE LA KERIO.

NA BENSON ASWANI
Katibu wa chama cha walimu nchini knut kaunti ya Baringo Joshua Cheptarus ameomba serikali ya kitaifa na ile ya kaunti kushugulikia swala la utovu wa usalama katika bonde la kerio kwani unaathiri pakubwa masomo ya wanafunzi haswa wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne.
Akiongea mjini Kabarnet, Cheptarus ameongezea kuwa kuendelea kufungwa kwa shule katika maeneo hayo kunarudisha chini viwango vya masomo na hivyo kuwa vigumu kumaliza silabasi inavyostahili huku walimu wakiwa na hofu ya kushambuliwa wakati wowote na wezi wa mifugo.
Aidha cheptarus amesema kuwa iwapo hali hiyo itaendelea basi wanafunzi ambao wako katika darasa la saba, kidato cha tatu na darasa la sita pia wataathirika pakubwa wakijitayarisha kufanya mtihani wao mwishoni mwa mwaka huu.