SERIKALI YATAKIWA KUIMARISHA USALAMA ENEO LA BONDE LA KERIO


Serikali imetakiwa kuchukulia kwa uzito swala la usalama katika bonde la kerio kwani shughuli za elimu zimetatizika pakubwa kutokana na ukosefu wa usalama eneo hilo.
Ni wito ambao umetolewa na wadau katika sekta ya elimu kaunti hii ya pokot magharibi wakiongozwa na naibu katibu mkuu wa chama cha walimu nchini knut tawi la pokot magharibi Raymond Kukotulia ambao wamesema wengi wa wanafunzi wamesusia shule kwa kuhofia usalama wao.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na msimamizi wa wadi ya Lomut Nelson Loturiang’iro ambaye amesema kuwa huenda shule eneo hilo zitafungwa kutokana na tatizo hilo la usalama.
Aidha ameelezea hofu kutokana na hali kuwa baadhi ya shule za eneo hilo zinatumika kama maeneo ya malisho ya mafugo ambapo wanaolisha mifugo hao kwenye shule hizo huwa wamejihami kwa bunduki hali ambayo ni hatari kwa usalama wa wanafunzi.