SERIKALI YATAKIWA KUIMARISHA USALAMA CHEPTULEL.

NA BENSON ASWANI
Chama cha walimu nchini KNUT tawi la Pokot magharibi kimeelezea wasi wasi kuendelea kuripotiwa utovu wa usalama eneo la Cheptulel mpakani pa kaunti hii na kaunti jirani ya Elgeyo marakwet.
Katibu mkuu wa chama hicho Martine Sembelo amesema kuendelea kuripotiwa visa hivyo kunaathiri pakubwa masomo katika eneo hilo na huenda kukaathiri mitihani ya kitaifa ambayo inatarajiwa kufanywa mwezi machi mwaka huu iwapo hali haitashughulikiwa.
Sembelo ameitaka serikali kuchukua hatua za dharura kushughulikia hali ya usalama eneo hilo kwa kuhakikisha kuwa kila shule inalindwa na maafisa wa usalama ili kuhakikisha wanafunzi wanaendelea na masomo bila tatizo jinsi ilivyo kwa wanafunzi wa maeneo mengine nchini.