SERIKALI YATAKIWA KUIMARISHA MSAKO DHIDI YA CAROLYNE KANGOGO.


Serikali imetakiwa kufanya juhudi zaidi za kumnasa afisa wa polisi mtoro Carolyne Kangogo ili kuwahakikishia wakenya usalama wao.
Baadhi ya wakazi mjini makutano katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameelezea kusikitishwa na hali kuwa kufikia sasa serikali imeshindwa kumtia mbaroni afisa huyo ambaye tayari amewaua watu wawili wakisema huenda akatekeleza mauaji zaidi iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa kumnasa.
Wakazi hao wameshutumu idara za uchunguzi nchini kwa kuchukua muda kubaini aliko Kangogo licha ya kuwa Kenya ni moja ya mataifa ambayo yanatajwa kuwa vitengo vya hali ya juu vya upelelezi.