SERIKALI YATAKIWA KUHARAKISHA MPANGO WA UOTAJI FEDHA KWA SHULE.


Mbunge wa Kapenguria katika kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Moroto ametoa wito kwa serikali kupitia wizara ya elimu kuharakisha mpango wa utoaji fedha ili kuwezesha shughuli katika shule mbali mbali kaunti hii.
Akizungumza na kituo hiki, Moroto amesema kuwa shughuli nyingi katika shule hizo zimekwama kutokana na uhaba wa fedha.
Aidha Moroto ameitaka tume ya huduma kwa walimu TSC kutuma walimu zaidi katika shule za kaunti hii, wakati uo huo akitaka utendakazi wa walimu hao kufuatiliwa kwa madai kuwa baadhi ya walimu wanaotumwa kaunti hii hawatekelezi majukumu yao inavyopasa.
Wakati uo huo Moroto ameitaka serikali kuwapa ajira vijana ambao wamesomea taaluma ya ualimu katika kaunti hii ili kusaidia katika kutoa huduma kwani wapo wengi ambao walimaliza masomo yao ila bado hawajapata ajira.