SERIKALI YATAKIWA KUGATUA UTOAJI FEDHA KWA WAZEE.


Mwakilishi wadi mteule ambaye pia ni kaimu kinara wa kiongozi wa wachache katika bunge la kaunti ya Trans-nzoia Magret Sabina Wanjala amepongeza serikali kuu kupitia kwa wizara ya jinsia kwa kutoa fedha za kuwasadia wazee chini ya mpango wa fedha kwa wazee, akisema zitawasaidia wazee hao haswa wakati huu mgumu wa janga la covid 19.
Sabina ambaye pia ametangaza kuwania kiti cha useneta kaunti ya Trans nzoia ametaka idara husika kugatua huduma ya utoaji wa fedha hizo hadi mashinani ilikuepusha wazee hao kusafiri mwendo mrefu kupokea fedha hizo,kwani wengi wao huporwa au kugharamika pakubwa pia ikizingatiwa masharti ya wizara ya afya ambapo wazee hao wako kwenye hatari ya maambukizi.
Aidha Sabina ameelezea malalamishi ya baadhi ya wazee hao kuhusu hatua ya fedha zao kupunguzwa kinyume na wanavyostahili kupata haswa fedha hizo zinapocheleweshwa, akitaka kaunti kamishna Sam Ojwang kuwawajibisha maafisa husika ili waelezee ni kwa njia gani fedha hizo hupunguzwa nani kwa nini.