SERIKALI YATAKIWA KUDHIBITI USALAMA MIPAKANI PA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI NA ELGEYO MARAKWET.
Viongozi kutoka kaunti ya pokot magharibi sasa wanaitaka serkali kuingilia kati na kudhibiti hali ya usalama katika eneo la kaunti za baringo pokot na elgeyo marakwet ili kuhakikishia wakaazi wa maeneo hayo usalama wa kutosha
Wabunge wiliam kamket wa tiati na mwenzake wa sigor peter lochakapong sasa wanaonya huenda hali ikawa mbaya zaidi ikiwa serkali haitaingilia kati na kurejesha hali ya utulivu katika maeneo husika
Lochakapong na kamket wamewatahadharisha viongozi kutoka eneo hilo dhidi ya kutoa matamshi yanayoweza kuchochea chuki badala yake kueneza amani ili jamii za eneo hilo ziweze kuishi kwa njia ya amani.