SERIKALI YATAKIWA KUARAKISHA UTOAJI WA HATI MILIKI KWA WAKAZI WA CHEPCHOINA.


Ipo haja kwa serikali kuharakisha shughuli za ugavi na utoaji wa hatimiliki ya ardhi kwa wenyeji wa Chepchoina eneo bunge la Endebess Kaunti ya Trans Nzoia, ambayo kwa muda mrefu wenyeji wamekuwa wakilumbana kutokana na mzoo wa umiliki wa ardhi hiyo.
Akihutubu eneo la Nauyapong baada ya kuidhinishwa kuwa mmoja wa viongozi wa jamii ya Pokot Moses Masinde Ainea amesema jamii mbalimbali wanaoishi eneo hilo wameendelea kuishi kwa uchochole kutokana na ukosefu wa hati miliki hizo, jambo ambalo limepelekea wao kuishi kama maskwata kwenye ardhi zao.
Aidha Masinde amelalamikia ugumu wa wenyeji eneo hilo kupata huduma muhimu za serikali kutokana na ukosefu wa vitambulisho, jambo ambalo anasema limechangiwa na eneo hilo kuwa mipakani mwa Kaunti ya Trans Nazoia na ile ya Pokot magharibi mbali na taifa jirani la Uganda.