SERIKALI YASHUTUMNIWA KWA KUSHINDWA KUDUMISHA USALAMA BARINGO.
Viongozi katika kaunti ya Baringo wameishutu serikali kuu kwa madai ya kushindwa kutafutia suluhu ya kudumu tatizo la ukosefu wa usalama kwenye baadhi ya maeneo ya kaunti hiyo.
Wakiongea kwenye eneo la lamaiywe, katika wadi ya mochongoi, eneo bunge la baringo kusini kwenye hafla ya kuombea amani, viongozi hao wamesema kuwa licha ya tatizo hilo kuwapo kwa muda, serikali imefeli kuwahakikishia wakazi usalama wao.
Wakiongozwa na mbunge wa eneo hilo charles kamuren, gavana stanley kiptis, mwakilishi akina mama gladwey cheruiyot miongoni mwa wengine, wameitaka serikali kuanzisha oparesheni ya kuwakabili wezi wa mifugo kama ilivyofanyika katika kaunti ya laikipia.
Viongozi hao aidha wamesisitiza kwamba utovu wa usalama kwenye eneo bunge la baringo kusini na kaskazini pamoja na eneo la bonde la kerio utakabiliwa iwapo serikali itawaajiri waafisa wa polisi wa akiba NPR.
Kwa upande wake mbunge wa baringo kaskazini william cheptumo amesema kuwa serikali inastahili kuanza kuwalipa fidia waathiriwa wote wa uvamizi uliotekelezwa na washukiwa wa wizi wa mifugo.
Hafla hiyo imeandaliwa siku moja tu baada ya wezi wa mifugo kuvamia eneo hilo na kuwajeruhi watu wawili kwa kuwapiga risasi.