SERIKALI YASHUTUMIWA KWA KUWAFURUSHA WAKAZI KATIKA ARDHI YA CHEPCHOINA.
Baadhi ya wakazi katika ardhi yenye utata ya Chepchoina katika mpaka wa kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti ya Trans nzoia waliofurushwa katika ardhi hiyo wameendelea kulalamikia masaibu wanayopitia baada ya makazi yao kubomolewa.
Wakiongozwa na Annah Edu wakazi hao wanadai kumiliki ardhi hiyo kihalali baada ya kukabidhiwa na utawala wa aliyekuwa rais mstaafu hayati Daniel Arap Moi mwaka 1994 wakishutumu hatua ya kubomolewa makazi yao katika shughuli iliyosimamiwa mashirikishi wa utawala wa bonde la ufa George Natembeya.
Wakazi hao sasa wanatoa wito kwa serikali kuangazia hatima yao kwani kwa sasa wanapitia hali ngumu hasa ikizingatiwa wanao walilazimika kukatiza masomo, huku wengi wao wakiishia kuishi kambini.
Ni hali ambayo imeshutumiwa na mbunge wa Kapenguria Samwel moroto ambaye amedai ardhi hiyo imetwaliwa na mabwenyenye huku akitaka mashirika ya kijamii kuingilia kati kutetea haki za wakazi hao. Moroto