SERIKALI YAOMBWA KUINGILIA KATI NA KUTATUA SUALA LA UKOSEFU WA USALAMA ENEO LA TUWAN KAUNTI YA TRANSNZOIA


Kufuatia kukithiri visa vya watu kubakwa na kushambuliwa kwa panga na wizi kutekelezwa katika mitaa ya mabanda ya Tuwan na Mitume kaunti ya Trans nzoia, kiranja wa wengi katika bunge la kaunti hiyo Benard Wambwa amevirai vyombo vya usalama kuzidisha doria nyakati za usiku na kuwatia nguvuni washukiwa.
Akirejelea kisa ambapo mama mmoja alibakwa na watu wawili kujeruhiwa kwa kukatwa kwa panga, Wambwa amesema kuwa ni sharti maisha ya wakazi wa maeneo hayo yalindwe.
Wakazi wa maeneo hayo wamesema kuwa wanaishi kwa hofu ya kushambuliwa na genge hatari ambalo limejihami kwa visu, mitaimbo na panga.