SERIKALI YAOMBWA KUINGILIA KATI NA KUREJESHA NGUVU ZA UMEME ENEO LA CHEMELEI KAUNTI HII YA POKOT MAGHARIBI


Wakazi wa eneo la chemelei kaunti hii ya Pokot magharibi wamelalamikia ukosefu wa umeme eneo hilo hali wanayosema kuwa imewapelekea kukwama shughuli zao nyingi.
Changamoto ya nguvu za umeme katika eneo la chemalei wadi ya lomut imesababisha kusimamishwa kwa biashara katika eneo hilo kwani wao wamebaki nyuma kimaendeleo jambo ambalo wanarai mjumbe wa sigor Peter lochakapong kuingilia kati tatizo hilo.
Na huku wakikabiliwa na msimu wa ukame wakaazi hawa aidha wanaomba gavana lonyangapuo kuwasaidia kuwaletea chakula cha kimsaada ili kujimudu kimaisha.
Wameomba pia kuwepo kwa usalama wa kutosha katika eneo la chesegon wakati huu wanafunzi wanapojiandaa kwa mitihani yao ya kcpe na kcse.