SERIKALI YAOMBWA KUINGILIA KATI KWA HARAKA NA KUOKOA FAMILIA MOJA ENEO LA KAPTAMA MLIMA ELGON KAUNTI YA TRANSNZOIA


Na Benson Aswani
Zaidi ya Wakaazi Alfu mbili waliofurushwa kutoka katika shamba la serkali la Kapsang iliyoko mpakani mwa kaunti ya Transnzoia na wadi ya Kaptama eneobunge la mlima elgon wanatoa wito kwa Serikali ya kitaifa kuwapa makaazi mbadala baada ya nyumba na mali zao kuchomwa na Maafisa wa Misitu
Wanasema kuwa baada ya wao kufurushwa katika Shamba hilo na Maafisa wa misitu katika kituo cha Sossio huku wakilazimika kulala nje baada ya Nyumba zao kuchomwa huku wakihangaishwa na Wanyama pori usiku kucha.
Wanasema kuwa hadi tunavyoenda hewani baadhi ya Watoto wao walipotea kufuatia zoezi hilo lililowaacha wenyeji katika hali mbaya ya kiafya wakiongeza kuwa kiwango cha Elimu kimedidimia baada ya Shule zilizokuwa katika eneo hilo kuharibiwa.
Naye Violet Magwilu mmoja wa afisa kutoka katika Shirika moja lisilokuwa la kiserkali ametaka serkali kujali maisha ya wananchi hao ambao wanaishi chini ya miti baada ya nyumba zao kuchomwa.