SERIKALI YAOMBWA KUINGILIA KATI KWA HARAKA NA KUHAKIKISHA HALI YA USALAMA INAIRIMARISHWA ENEI LA CHESOGON KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI


NA BENSON ASWANI
Visa vya utovu wa usalama eneo la chesogon mpakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jirani ya Elgeyo Marakwet vimeendelea kuripotiwa.
Hii ni baada ya wavamizi wanaoaminika kutoka eneo la Marakwet mashariki kuvamia eneo hilo hiyo jana na kumjeruhi vibaya mkazi mmoja wa eneo hilo ambaye anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Kapenguria kaunti hii.
Tito Rotino ni mkazi wa eneo hilo la chesogon.
Wakazi hao wameshutumu idara ya usalama kwa utepetevu wakidai polisi walichukua muda mrefu kushughulikia hali hiyo, wakitaka serikali kuchukua hatua kudhibiti hali hasa katika shule mbili za eneo hilo zinazodaiwa kutumika na wavamizi kutekeleza uhalifu.