SERIKALI YALAUMIWA KWA UTOVU WA USALAMA UNAOSHUHUDIWA CHESOGON.


Waziri wa usalama wa ndani ya nchi Dkt Fred Matiangi ametakiwa kuhakikisha anatekeleza ahadi aliyotoa kwa wakazi wa eneo la chesogon mpakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jirani ya Elgeyo marakwet ya kujengwa kituo cha polisi eneo hilo.
Gavana wa kaunti hii ya pokot magharibi John Lonyangapuo amesema kuwa serikali imechukua muda mrefu kutekeleza ujenzi wa vituo hivyo huku wakazi wakiendelea kuuliwa na wahalifu ambao wanaendeleza visa vya uvamizi eneo hilo.
Kwa upande wake kamishina wa kaunti hii Apolo Okelo amesema kuwa idara ya usalama kaunti hii kwa ushirikiano na serikali ya kaunti inatarajiwa kuanzia leo kuweka mikakati ya kuweka kituo cha muda cha maafisa wa polisi eneo hilo ili kuhakikisha utulivu unaafikiwa.