SERIKALI YAHIMIZWA KUWAPA VIJANA VITAMBULISHO


Viongozi wa vyama tofauti vya kisiasa katika kaunti ya Kakamega wanaitaka serkali kupitia idara ya usajili wa watu kuhakikisha imeweka mikakati ya kuwapa watu Vitambulisho vya kitaifa ambayo imeripotiwa kurundika ofisini hasa wakati huu ambapo shughuli ya usajili wa wapiga kura imeanza rasimi.
Kulingana na mshirikishi wa chama cha Anc katika eneobunge la malava Patrick Butalanyi vitambulisho vya watu wengi vimerundikana katika afisi za usajili wa watu kwa sababu havijachukuliwa na wenyewe.
Butalanyi anasema ni wajibu wa Serkali kuhakikisha wahusika wanapewa Stakabadhi hizo muhimu hasa wakati huu wa zoezi la usajili iliwashiriki kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Wakati uo huo mshirikishi wa chama cha Uda katika eneobunge la lurambi jeff mwenje ameitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini iebc kuongeza muda wa zoezi la usajili wa wapiga kura ilikuwapa wakenya fursa na haki yao ya kushiriki kwenye uchaguzi