SERIKALI YAENDELEZA MCHAKATO WA KUTATUA MIZOZO YA ARDHI KACHELIBA.

Serikali inaendeleza shughuli ya kutatua mizozo inayohusu ardhi ambayo imekuwepo kwa muda sasa hasa kupitia kugawa baadhi ya vipande vya ardhi kwa wakazi katika eneo la Kacheliba kaunti hii ya Pokot magharibi.
Akizungumza na kituo hiki naibu kamishina eneo la Kacheliba Fredrick Ndubi amesema kuwa mchakato huo unaendelea kukamilika katika baadhi ya maeneo eneo hilo akiahidi kusuluhishwa mizozo ambayo imelemaza shughuli hiyo katika baadhi ya maeneo.
Aidha Ndubi amesema kuwa wizara ya ardhi inasubiriwa kuweka katika gazeti rasmi la serikali majina ya wakazi wa maeneo ya Orolwo, Lokichar na kalimng’orok ili kupisha shughuli ya kugawa ardhi hatua itakayosuluhisha mizozo ambayo inashuhudiwa.
Wakati uo huo Ndubi ametoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo kukumbatia njia zilizopo za kisheria katika kusuluhisha mizozo ya ardhi ili kuzuia vurugu ambazo huenda zikapeleka kuharibiwa mali na kusababisha hasara.

[wp_radio_player]