SERIKALI YAENDELEA KUWEKA MIKAKATI MKUKABILI UKAME.


Serikali imeendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa wakazi wa maeneo yaliyoathiriwa na ukame wanapata msaada unaohitajika.
Akizungumza na kituo hiki katibu katika wizara ya hudumna za umma, jinsia na mipango maalum Mika Powon amesema kuwa serikali inashirikiana na wadau wengine kukabiliana na ukame hasa baada ya kutangazwa janga la kitaifa, ikiwemo kutenga fedha za kushughulikia hali hii.
Wakati uo huo Powon amesema kuwa kaunti hii ya Pokot magharibi haijaathirika pakubwa na ukame ikilinganishwa na kaunti hasa zinazopatikana maeneo ya kaskazini mashariki na baadhi ya kaunti za pwani.