SERIKALI YAAHIDI KUWEKA MIKAKATI YA KUWALINDA WAATHIRIWA WA DHULUMA ZA KIJINSIA.

Waathiriwa wengi wa dhuluma za jinsia hasa watoto wanakosa kuripoti visa hivyo kutokana na hofu ya kukabiliwa na washukiwa.

Akizungumza mjini Kitale kaunti ya Trans nzoia, katibu mwandamizi katika wizara ya huduma za umma na maswala ya jinsia Rachael Shebesh amesema serikali inaweka mikakati ya kutoa usalama kwa waathiriwa hao ambao watatoa ripoti kuhusu dhuluma hizo.

Kwa upande wake kamishina wa kaunti ya Trans nzoia Sam Ojwang ameelezea haja ya kuwepo ushirikiano wa karibu baina ya taasisi za usalama na idara ya mahakama kuzuia watakaopatikana na makosa ya kuendeleza dhuluma za kijinsia kuachiliwa kwa dhamana.