SERIKALI YA UINGEREZA YAAHIDI KUIMARISHA USHIRIKIANO NA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI.

Serikali ya uingereza kupitia serikali kuu, ina fahari kushirikiana na serikali ya kaunti hii ya Pokot magharibi katika kuhakikisha kuwa maendeleo yanaafikiwa kwa manufaa ya mwananchi.

Akizungumza mjini makutano katika ziara ya siku mbili kaunti hii ya Pokot magharibi kukagua miradi ya maendeleo ambayo inafadhiliwa na benki ya dunia, mkuu wa idara ya kimataifa ya maendeleo DFID Ben Fisher amesema serikali hiyo itaendelea kupitia benki ya dunia kufadhili miradi hiyo.

Amepongeza miradi ambayo tayari imetekelezwa katika kaunti hii ambayo  wamezuru ikiwemo kitengo cha wagonjwa mahututi ICU katika hospitali ya Kapenguria pamoja na miradi kadhaa ya kilimo hali anayoitaja kuwa matunda ya ugatuzi.

Kwa upande wake gavana wa kaunti hii John Lonyangapuo amepongeza serikali ya uingereza kwa ufadhili ambao imeleta kaunti hii, akiahidi kuendelea kushirikiana nayo kwa pamoja na benki ya dunia ili kufanikisha maendeleo zaidi.