SERIKALI YA TRANS NZOIA YAWEKA MIKAKATI YA KUKABILI MABADILIKO YA TABIA NCHI.


Wizara ya maji mazingira na mali asili katika kaunti ya Trans Nzoia imetenga bajeti ya shilingi Milioni 20 kwa upanzi wa miti na utunzaji wa mazingira kama njia moja ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya anga nchini.
Akihutubu mjini Kitale baada ya kuongoza hafla ya kuadhimisha siku ya mianzi ulimwenguni iliyoandaliwa katika makavazi ya kitaifa mjini Kitale waziri wa mazingira Kaunti ya Trans Nzoia Andrew Musungu amesema mianzi ina manufaa mengi kwa mazingira na tayari wizara yake imeagiza miche 5000 ya mianzi itakayo pandwa kwenye vyanzo vya maji na kando kando ya ya mito.
Kwa upande wake mshirikishi wa muungano wa wanautalii Kaunti ya Trans-Nzoia Sarah Musundi amesema sekta ya Utalii na utunzaji wa mazingira zinaambatana hivyo ipo haja ya ushirikiano ili kupiga jeki sekta hizo mbili kwa pamoja.