SERIKALI YA TRANS NZOIA YASUTWA KUFUATIA HUDUMA DUNI KATIKA VITUO VYA AFYA.


Mwenyekiti wa wafanyakazi Kaunti ya Trans Nzoia Samuel Juma Kiboi amelalamikia ukosefu wa dawa na vifaa muhimu vya kutoa huduma za afya katika vituo vya afya Kaunti hiyo jambo ambalo limepelekea kudorora kwa utaoji wa huduma za afya kwa umma katika hospitali ya rufaa mjini Kitale.
Kwenye mkao na wanahabari afisini mwake Kiboi amelaumu usimamizi mbaya wa wizara hiyo akitaka Gavana Patrick Khaemba kufanya mabadiliko katika usimamizi wa idara hiyo akiongeza kuwa wagonjwa wanapitia wakati mgumu kupokea huduma za afya kutokana na kukosekana dawa na vifaa vingine muhimu hopsitalini humo.
Wakati huo huo Kiboi amemtaka mwakilishi wa wadi ya Kaplamai Elkana Manjari kuelezea jinsi alivyo tumia zaidi ya shilingi Milioni 100 fedha za utekelezaji maendeleo katika wadi au ward specific fund, akisema wenyeji eneo hilo hawajafaidi fedha hizo kwani hawajaona miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na fedha hizo.