SERIKALI YA TRANS NZOIA YASHUTUMIWA KWA KUWATELEKEZA WAHUDUMU WA AFYA

Mwenyekiti wa wafanyakazi kaunti ya Trans-nzoia Samuel Kiboi ameshutumu vikali serikali ya kaunti hiyo kupitia wizara ya afya kwa kile ametaja kukosa kuwalipa marupurupu ya kufanyia kazi katika mazingira magumu wahudumu wa afya wakati huu wanapokabiliana na janga la covid 19.

Kwenye mkao na wanahabari Kiboi ametaka gavana wa kaunti ya Trans-nzoia patrick khaemba kuwajibisha afisa mkuu wa wizara ya afya charles barasa ili kuelezea matumizi ya fedha hizo kwani wahudumu hao hawajapokea marupurupu yao tangu kuzuka kwa janga la corona.

Aidha Kiboi amelalamikia ubadhirifu wa fedha za kuwanunulia sare za kazi askari wa kaunti hiyo akisema tangu mwaka wa 2019 hawajapokea sare zao licha ya fedha kutengwa, vilevile akitaka uchunguzi kufanywa kwa fedha za kufadhili elimu ya ziada kwa wafanyakazi wa kaunti hiyo akiongeza kuwa ni wachache mno wanaofaidi ufadhili huo licha ya kaunti kuwa na zaidi ya wafanyakazi alfu 3000.