SERIKALI YA TRANS NZOIA YASHUTUMIWA KWA KUWAHANGAISHA WAFANYIBIASHARA.


Siku moja tu baada ya kushuhudiwa makabiliano baina ya wafanyibiashara na maafisa wa polisi mjini Kitale kaunti ya Trans nzoia, mwakilishi kina mama katika kaunti hiyo Janet Nangabo ameshutumu uongozi wa gavana Patrick Khaemba kwa kile amedai kuwahangaisha wafanyibiashara.
Nangabo amesema kuwa wafanyibiashara wengi mjini Kitale wamelazimika kuchukua mikopo kuendeleza biashara zao kufuatia changamoto ambazo zimesababishwa na janga la corona na inasikitisha kuona serikali ya kaunti ikiwahangaisha.
Aidha Nangabo amesema wafanyibiashara hao wameendelea kuhangaishwa licha kulipia leseni zao za kufanyia biashara akisema kuwa huenda hali hii ikapelekea ongezeko la uhalifu kaunti hii iwapo serikali hiyo haitaweka mikakati ya kushughulikia swala hilo.
Maandamano hayo yalipelekea kutiwa nguvuni mwenyekiti wa wafanyibiashara kaunti hiyo martine waliaula kwa madai kuwa aliongoza maandamano hata baada ya kunyimwa idhini.