SERIKALI YA TRANS NZOIA YASHUTUMIWA KWA KUKITHIRI UFISADI.


Aliyekuwa mratibu wa utawala eneo la bonde la ufa George Natembeya ambaye ametangaza nia ya kuwania kiti cha ugavana katika kaunti ya Trans nzoia ameahidi kuimarisha maenedeleo katika kaunti hiyo kwa kukabili ufisadi ambao amesema umekithiri.
Natembeya ambaye anawania kiti hicho kupitia tiketi ya chama cha DAP-K amesema kuwa ufisadi umekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo katika kaunti hiyo.
Natembeya amesema kuwa japo ataridhi serikali iliyo na madeni mengi iwapo atachaguliwa kuongoza kaunti hiyo ataimarisha uhusiano na serikali kuu kuhakikisha kuwa mwenyeji wa kaunti hiyo ananufaika na miradi ya maendeleo.
Wakati uo huo Natembeya amesema kuwa serikali yake itawekeza katika viwanda katika juhudi za kuwasaidia wakulima wa mahindi na wafugaji ili kuimarisha shughuli za kilimo na kuhakikisha umasikini unapungua miongoni mwa wakazi wa kaunti hiyo ya Trans nzoia.