SERIKALI YA TRANS NZOIA YAENDELEZA MIKAKATI YA KUIMARISHA SEKTA YA UTALII.

Naibu Gavana Kaunti ya Trans Nzoia Philomena Kapkory amesema serikali ya Kaunti ya Trans Nzoia imeweka mikakati kupiga jeki sekta ya utali.

Akihutubu kwenye maadhimisho ya siku ya utalii nchini Philomena amesema Kenya ilipokea shilingi  B156.5 kutoka kwenye sekta ya utali hivyo Kaunti ya Trans Nzoia inafaa kuwa miongoni mwa Kaunti zitakazofaidi fedha hizo kupitia utalii.

Tunataka kuifanya kaunti ya Trans nzoia kuwa kitovu cha utalii eneo hilo. Tuna kibarua cha kufanya kuhakikisha kwamba tunaitangaza Trans nzoia kama kivutio cha utalii kwa sababu tuna vivbutio vingi kwenye kaunti hii ambavyo vinaweza kuifanya iwe miongoni mwa maeneo ambayo yanwavutia watalii wengi hata wa kimataifa.” Alisema.

Kwa upande wake waziri wa Utalii Kaunti ya Trans Nzoia Aggrey Chemonges amesema maambukizi ya Covid 19 yaliathiri pakubwa sekta hiyo hivyo wizara yake kwa ushirikiano na washikadau katika sekta hiyo wameanzisha mikakati ya kuikwamua.

“Ugonjwa wa Covid 19 ulituathiri zaidi ila kama serikali ya kaunti tumeweka mikakati ya kuboresha utalii na tutajitahidi tuwezavyo kuhakikisha kwamba mbuga zetu za Saiwa na Mlima Elgon zinafikiwa na watalii. Alisema.