SERIKALI YA TRANS NZOIA YAANZISHA MPANGO WA KUWACHANJA WATOTO.
Na Benson Aswani
Zaidi ya 80% ya watoto katika Kaunti ya Trans-Nzoia walikosa kupokea chanjo zao za mwaka wa 2020 kutokana na kuzuka kwa janga la Covid 19 miongoni mwa vigezo vingine kwa mujibu wa afisa wa uhamasisho wa maswala ya Afya Kaunti ya Trans-Nzoia Leah Okumu.
Aidha Okumu ameelezea umuhimu wa chanjo hizo miongoni mwa watoto akisema wamezindua mpango wa kuwatafuta watoto waliokosa chanjo hizo kwa siku 100 zijazo wakilenga kuafikia 70% ya utoaji wa chanjo ya saratani ya uzazi ya HPV kwa watoto wasichana wenye umri wa miaka 10-14.
Kwa upande wake Msimamizi mkuu wa maswala ya utoaji wa chanjo katika Kaunti ya Trans-Nzoia Angeline Atieno amesema kupitia kwenye mpango wa wizara hiyo wanalenga kuafikia zaidi ya watoto 66,433 Kaunti ya Trans-Nzoia.