SERIKALI YA TRANS NZOIA YAANZA KUTEKELEZA MPANGO WA UHC.


Wizara ya Afya Kaunti ya Trans Nzoia imezindua mpango wa kuwasajili wenyeji 18,546 kwa njia ya kielectroniki watakaonufaika na mpango wa afya kwa wote, universal health care kwa ushirikiano na serikali ya Kaunti na serikali kuu chini ya bima ya afya ya kitaifa NHIF.
Kwenye mkao na wanahabari wakati wa uzinduzi huo waziri wa afya Kaunti ya Trans-Nzoia Clare Wanyama amesema mpango huo wa bima ya afya ya UHC unalenga familia za wasiojiweza katika jamii ambapo usajili wa waliochaguliwa umezindulliwa hiyo jana.
Kwa upande wake mkurugenzi wa kanda ya bonde la uffa Otom Robert amesema mpango huo wa afya unaenda kupiga jeki pakubwa utoaji wa huduma za afya kaunti hiyo kwani gharama ya huduma ya afya itasalia kwenye hospitali husika.
Mwenyekiti wa kamati ya Afya katika bunge la kaunti ya Trans-Nzoia ambaye pia ni mwakilishi wadi ya Statunga Daniel Kaburu amesema utekelezaji wa mpango huo utakuwa afueni kwa wenyeji Kaunti hiyo kwani utawapunguzia gharama ya kila siku ya michango kwa ajili ya malipo ya huduma za afya kutoka kwa umma.