SERIKALI YA TRANS NZOIA NZOIA YASUTWA KWA KUONGEZEKA UNYAKUZI WA ARDHI


Mwenyekiti wa mashirika yasiyo ya serikali kaunti ya Trans nzoia Kefa Were ameelezea kughadhabishwa na kuendelea kuongezeka visa vya unyakuzi wa ardhi za umma ikiwemo ya makaburi mtaani kibomet mjini kitale.
Akizungumza na wanahabari Were amesema kuwa afisi yake imepokea stakabadhi muhimu ambazo zinaonyesha namna baadhi ya maafisa wakuu wa kaunti hiyo wanavyotumia njia za mkato wakilenga kupata hati miliki za sehemu hiyo iliyotengewa makaburi.
Were ametoa wito kwa idara ya upelelezi na tume ya kitaifa ya ardhi kuchunguza baadhi ya maafisa wa idara ya ardhi katika kaunti ya trans nzoia na kuwafungulia mashitaka kwa mujibu wa sheria.

[wp_radio_player]