SERIKALI YA POKOT MAGHARIBI YATAKIWA KUSHUGHULIKIA SWALA LA BARABARA ENEO LA CHEMAKEU


Wakazi wa eneo la Chemakeu katika wadi ya Riwo kaunti hii ya Pokot magharibi wametoa wito kwa serikali ya kaunti kupitia idara ya barabara kukarabati daraja linalounganisha eneo la Chemakeu na Cherangan.
Wakazi hao wamesema kuwa kwa sasa daraja hilo limeonyesha dalili za kukatika na huenda ikawa hatari kwa wakazi wanaotumia barabara hiyo hasa wakati huu ambapo kumeanza kushuhudiwa msimu wa mvua.
Wakati uo huo wakazi hao wametaka kujengwa barabara za eneo hilo ili kufanya rahisi kwa wakazi kufikia huduma muhimu kwani ilivyo sasa ni vigumu hasa kwa kina mama wajawazito kufikia vituo vya afya.